My First Love Letter

Sorry for all the non-Swahili speakers,  and readers for that matter.  This post will be in Kiswahili. And I shall not be translating. I remember there was a post that Modo did in Kiswahili and that inspired me to try my mine; after all, I learnt Kiswahili for at least 12 years.

4B Class, 2005

4B Class, 2005

Nikiwa kidato cha nne, mwaka wa 2005, nilikiwa msichana mtukutu sana. Nakumbuka siku moja tukimsengenya mwalimu wetu wa Tarakilishi.
“Jana nilipitia hiyo njia iliyo karibu na nyumba za waalimu…” kaanza M.T.

“Halafu?” Tukamwuliza.

“Nikaona dame mmoja amevaa suruali moto moto akianika shati za buluu, ukipenda samawati. Na sote tunajua nani huvaa shati za buluu…”

“Suruali moto moto?”

“Hot pants.”

“Kisha?”

“Wacha msichana kugeuka, uso wake kajaa madoa doa, mengine yana vichwa vieusi….”

Vicheko vikatushika. Kutoka hapo nikaelekea maktaba kuenda kusoma. Kawaida yangu huwa sisomi lakini mtihani wa mwisho (KCSE) ulikuwa wakaribia. Nilikiwa msomaji wa riwaya, kama vile vitabu  vya Mills n Boon, na waandishi wengine kame vile John Grisham, Danielle Steel, Sidney Sheldon, Ken Follet, Jackie Collins na wengine wengi. Lakini wakati huu nikidhubutu kuvifungua, mawazo yananijia najiuliza maswali kama vile: “Eleze kwa kutumia michoro, jinsi Kames na Eskers zinavyotendeka. Alama 15 . (Kwa wale hawafahamu, Kames na Eskers hupatikana katika somo la Jografia). Riwaya hizi nazitupilia mbali nachukua vitabu vya Jografia na kutia bidii.

Siku moja nikitoka maktaba na rafiki yangu Chumba, huku tukipeleka vitabu darasani ili tuelekee mlo wa jioni, tukaona kijana mmoja barobaro akisimama mlangoni wa ofisi za waalimu. Chumba aliyekuwa wa kwanza kumwona akaniambia “Savvy tuende tumsalimie.” Kawaida, wavulana huwa nadra sana, kwani shule yetu ilikuwa ya wasichana pekee. (PinkM anaweza kukuelezea pia.) Kwa hivyo mvulana kama yule tuliyeona ni kama kumpa Obama urais wa Marekani.

“Mimi sitaki kumsalimu, kama wewe wataka nenda.” Nikamjibu Chumba.

“Savvy we muoga, tangu lini..” akakejeli Chumba.

Nami kwa vile sikuwa nataka kuonekana muoga, nikashika njia kuelekea ofisi. Kufika hapo, nikamwona kwa karibu kijana huyo. Alikuwa amevaa fulana ya kijani kibichi iliyo na kofia. Hakuwa mweusi wala mweupe sana, tuseme kahawa hivi. Sura ya kawaida, nisemeje!  Nikasema hello kisha nikamwuliza:

“Umeoana, um..um…” Nikageuka kwuliza Chumba anisaide, lakini wapi! Alikuwa katoweka.

“Umeona Mista Bunguswa?”

“Aa.”

Kusikia hivyo nikaanza mwendo wa pole pole kwelekea jumba la maankuli, nikajizua kukimbia. Ningekuwa mzungu uso wangu ungekuwa mwekundu. Kufika huko, nikapata Chumba ashaketi anakula, nami nikajitilia chakula kisha nikaketi na kumwuliza kwa nini alitoroka. Kabla hajanijibu, maswali nikatupiwa kutoka kila kona ya meza:

“Savvy twambie juu ya kijana wako.” MT akaanza.

“Sio kijana wangu.”

“Eh Savvy! Hatutaku-‘slice’. Twambie tu, anaitwaje? Anasoma wapi? Anafanya nini hapa?”

“Nawaambua sijui…” Nikajibu kwa hasira kisha nikatoka nikaacha chakula changu hapo.

Hayo yakasaulika hadi siku nyingine tukitumia ‘stairs’ za maabara ya Kemistria, tukakutana na yeye. Nilikuwa na Chebet wakati huu. Tukasalimiana, kisha tukaanza kuongea mambo ya kawaida tukijuana. Akatuambia yeye husoma shule nyingine hapo karibu (nimesahau jina la shule hiyo), kisha huja kufunzwa masoma ya ziada na Mista Bunguswa. Alikuwa kidato cha tatu, nasi tukamwambia tuko kidato cha nne na tulikuwa karibu kufanya mtihani wetu wa mwisho. Akatutakia mafanikio. Tukamwambia kwaheri ya kuonana na kwenda zetu. Kabla ya kuondoka akatujulisha jina lake: Harrison.

Siku chache baadaye, nikapata barua isiyo na stampu. Kuifungua nikapata inatoka kwa Harrison mwenyewe. Nikamwita Chumba, Chebet, na pamoja na Vee, Kemy, Ciara na wengine wengi, nikaanza kuisoma. Hiyo ilikuwa barua yangu ya kwanza ya mapenzi. Ingawa nilikuwa mtukutu wa kuvunja sheria, wavulana sikuwapenda sana (sio kama siku hizi J ). Barua ilikuwa imejaa mistari ambayo kwa kiingereza ninaweza kusema ‘classic overused love lines’. Lakini ilikuwa na kasoro moja, makosa yaku-‘spell’ yalikuwa yamejaa. Nikaambiwa niyapuuze. Sikuwa najisikia kujibu barua hiyo, lakini darasa mzima ni kama lilikuwa likitaka nifanye hivyo.

Papo hapo Vee akachukua karatasi zake maridadi ambazo alikuwa anazitumia kuandikia Ibrahim (Ib) mashairi marefu ya mapenzi na kunipa. Kila mtu akanizingira nikianza kujibu barua. Nikachora mistari kama vile: “You are the Harrison Ford of my life…” na kuandika ma-‘dedications’ kama Strangers in the Night (Glen Washington), My Love (Westlife) na zingine za mtindo wa reggae, kwani kwa tamko la Chebet “Boy wako Savvy ni ghetto.” Sikukosa wa kumpelekea Harrison jibu langu; karibu darasa mzima lilijitolea.
Mtihani wa KCSE ukaanza. Wiki ya kwanza haikutupa nafasi ya kupumua, tulikwa na karatasi asubuhi na adhuhuri. Juma la pili nilikuwa sina karatasi zozote adhuhuri na nilikuwa nafika kidimbwini kila siku kuogelea (Sijui kama kilikuwa kimejengwa PinkM akiwa). Jioni siku moja, nikapata barua nyingine kutoka kwake Harrison.

Kama kawaida, darasa mzima likaja kusoma, kwani wakati huu, ilikuja na mauwa, ya aina ya ‘rose’ mekundu. Vee akatafuta chupa ya soda, akaijaza maji kisha akatia maua ndani. Kila mtu akaketi kimya tukaanza kusoma barua. Mistari ya mapenzi ikaongezeka, akaniambia hataki kunipoteza kwa vile nilikuwa naondoka baada ya mtihani, na kuniambia nimwachie nambari zangu za simu. Kisha ma-’dedications’ zingine. Nami nikaijibu barua hii, nikijua hata kama sikumpenda, siku yangu ya kuondoka ilikuwa yakaribia.
Barua ya tatu niliyoipokea haikuwa na mengi ya mapenzi. Ilikuwa fupi na alinipa nambari zake za simu, kisha akanipa hadithi juu ya simu yake kuharibika na kutaka kuniomba hela (elfu moja )ili aitengeneze. Aliahidi kunirudishia kabla sijaondoka.

Yote yakaishia hapo. Anawezaje kuniomba pesa? Kwani nilikuwa nakaa kama mtoto wake Kibaki? Au Mwiraria? Kwanza hizo namba zake za simu hazikuwa halali kwani zilikuwa: 07xx xx xx . Nane tu, badala ya nambari 10. Ama labda simu zile za kitambo (2005) zilikuwa za nambari nane. Sikuijibu barua hiyo. Hata marafiki zangu waliniambia “Savvy, mwangushe kama kiazi moto.” (Direct translation at work here: Drop him like a hot potato.)

Nakumbuka siku niliyokuwa nikiondoka. Mamangu alikuja na Peugot 504 ya samawati iliyokuwa ikiendeshwa na Kones. Tulipofika mahali ambapo barabara ilikuwa yakutana na njia kuu, tukingoja magari yapite, nikamwona kijana mmoja akitembea kuelekea lango kuu. Alikuwa kavaa fulana ya kijani kibichi. Akigeuka kuiangalia motokaa yetu, njia ikaisha magari tukaondoka tukiacha wimbi la moshi nyuma. Sijawahi kumwona Harrison tena. Barua zake nilizichoma tukiwa na “The Great Bonfire” –tulichoma vitabu vyetu tulisivyohitaji baada ya kumaliza mtihani.

Advertisements

23 Responses

 1. I would have loved to get a translation but then again not the same feeling I suppose….
  Anyway girl I thought of just taking this time to invite you and your friends to a quest for health and lose weight these coming weeks. Africa with style is running this campaign and we need as much support as we can get. Join us it will be so much fun the more the merrier…
  NICE blog you have here it very cosy…

  How do I join? Of course Africa is running with style, Pamela Jelimo for one…though someone said Ashley’s should spruce her up 🙂

 2. I had to read it aloud!

  Nipe maana ya maneno yafuatayo.
  Kames na Eskers

  Some Geographical features…am sure u could google that up..

  Barobaro

  A teenage boy..

  Then stairs ni ngazi kwa kiswahili, I think.

  Nikatumia ngazi za maabara ya Kemistria..sounds fake to me.

  • Naipenda sana hadithi yako na ningeoomba ujaribu kuingia katika sanaa ya uandishi.heko.ukitaka kunifikia nambari hii hapa0705778463.shukrani

 3. LOL @ ‘The Harrison Ford in my life”… I almost fell out of my chair.

  I used it fo real

  This post just reminded me how much I hated Swa in school.

  Reading Swa books was the biggest headache for me, I hated Fasihi. The only good book I have read was Ken Walibora’s Siku Njema.

 4. right. my swa is rusty as heck. it took me two days to read it but i am finally done.

  I admit Kiswahili is a tough read, and I did not even use Msamiati!

 5. I wanted to give up,it seemed long and as at now am sure my swahili is pathetic,but I got courage and read,i read it all!I even noticed some errors(najaribu kukutia hofu juu ya kiwango cha lugha yako!)I loved it.

  Kweli dada ulinishtua. Nilijaribu sana niandike bila makosa. Asante kwa kusoma.

  But Savvy,this Harrison Ford of your life come to your high school ,broke and imagined that you were the one to save him? A first love letter in Form four?A naughty you?well I will try to believe you!! At my time it was out of question to own a phone in school, lucky you ,lucky Harrison!

  Can you imagine he thought that, a whole Harrison Ford? Well, I may have been naughty, but tomboy like so no romantic boyfriends

 6. Hii post (what’s a post in Swa?) ilikuchukua muda gani kukamilisha? Ulifanyia kwa microsofti neno? Si ilishangaa sana hiyo microsofti neno na kuweka mstari mwekundu chini ya kila neno kwa ajili haielewi hiyo spelling?

  Mikrosofti neno ilikuwa nyekundu sana siku hiyo. Lakini dadangu Shiko, si waishi Mombasa. Unawasilianaje na majirani zako?

  Kiswahili sio Lugha yangu ya kwanza (First language) kwa hivyo kukisoma sio rahisi sana kwangu lakini nimejitahidi nikasoma post (what was it again in swa) yote.

  Lakini umenichekesha sana we…

 7. I had trouble reading this coz my Swahili is really wanting(Worst Subject in schooll for the 12 yrs).

  It was also my worst perfomance in KCSE.

  I did note the photos though:The Red Jerseys-.You must have schooled in Kottet(You are smart) or LCVR(You do know how to have fun).Cant be Msoh,or is it?

  Am both smart and also know how to have fun, but you are close to the truth. I’ll tell you though, Kottet.

 8. barua yako ya kwanza ya mapenzi ilinichekesha sana hasa hapo ambapo Chebet alikuacha peke yako ili utupe kiswahili,ka unaelewa maana.Damn! swa is difficult but ni kweli vile umekiri jinsi watu hubadilika wakiingia chuo kikuu.

  Kweli nimebadilika kwani nawapenda wavulana siku hizi 😉

 9. Aisee, dada. Umejaribu kweli! Umenirudisha hadi siku za kuandika insha. Jameni, siku ngumu hizo!!!

  Nina swali moja lakini…mbona kila upatapo barua ilikuwa lazima lisomwe na baraza la wamam..pole..wadada.

  I once used an edited excerpt from one of our course books(the play) to one of the ladies in your school, and the next thing I knew, half the fourth form class wanted to meet the letter writer at the next school function. Didn’t mind the attention, though.

 10. @ A son…

  Of course in high school, letters are universal. You may want to pick up points, get ideas..stuff like that. Unless you really loved the guy…then u share the letter. I remember there were some two chiquittas in our class who got a letter from the same guy…now imagine if they had never shown each other..the guy would not have been busted

  btw, we have a lecturer who calls the chicks in class: “nyinyi wamama”..and we all fume.

 11. i luv a gal and she loves me but my cousin is trying to break our love

 12. why is it that many guys hate swa.i hate reading swahili novels but i loved swahili.or is it because i finished high school last year n maybe u finished much earlier.even durin our love letters were qead aloud in front of class.THANKS

 13. The first one is the income that it generates. With an exhaustive range of luxury and contentment.
  If you truly want to explore, as well as its
  real estates, which developed paphos car hire into a haven for money
  laundering. We recently went through our operations to see where we could
  do in a week or for a number of flash points occurred.

 14. It’s appropriate time to make some plans for the longer term and it’s time to be happy.
  I’ve read this submit and if I may just I wish to recommend you few interesting things or advice. Perhaps you can write next articles regarding this article. I desire to read more things about it!

 15. Every weekend i used to pay a visit this web page, as i wish for enjoyment,
  since this this site conations actually fastidious funny data too.

 16. A’m a challi 25yrz old .I nid a galfrnd of 18 to 24yrs.I wak at TALA mrkt,job da pharmacy/Chemisty.
  MA DETAILZ ARE……..
  [0712735489]TRY PLIZ.

 17. xaxa ndoninn?au mwandishi umetuchoka

 18. Great goods from you, man. I’ve understand your stuff previous
  to and you are just extremely great. I really like what you’ve acquired here, certainly like what you are stating and the way in which you say it.
  You make it entertaining and you still take care of to keep it wise.
  I cant wait to read far more from you. This is actually a
  terrific web site.

 19. boiz aibu nayo..!

 20. I do not know if it’s just me or if perhaps everyone
  else experiencing problems with your blog.
  It appears like some of the written text in your content are running off the screen. Can someone else
  please provide feedback and let me know if this is happening to them too?
  This might be a issue with my web browser because I’ve had this happen before.

  Kudos

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: